Mawasiliano katika kufanikisha utendaji.

Naibu waziri wa ujenzi, mawasiliano na usafirishaji, mh. Moh’d ahmada, amesema mawasiliano kati ya viongozi na wanaowaongoza ni muhimu katika kufanikisha shughuli za kiutendaji ndani ya taasisi zao.

Amesema viongozi wataweza kuongoza vizuri katika taasisi zao endapo watazingatia maadili na kanuni za uongozi ambazo zinaelekeza kusikiliza ushauri kwa watendaji unaowaongoza.


Akifunga mafunzo kwa viongozi wa taasisi ya elimu ya juu ya vyuo vikuu zanzibar zahlife, mh. Ahmada, amesema jamii imekuwa na matumaini makubwa na wasomi kupitia taaluma zao, hivyo ni vyema kujijengea mazingiza ya uaminifu tokea wakiwa vyuoni.

Makamu mwenyekiti wa zahlife, latifa khamis juakali, amesema pamoja na matatizo mbali mbali yaliopo viongozi hao hawatokata tamaa katika kugombania nafasi za uongozi.katika jamii.
chanzo:Zbc.

Comments