
Juma Hija kombo mkaazi wa Mzambarau takao alisimulia tukio hilo
kwasimanzi akisema kuwa, yeye pamoja na mkewe Moza Kombo majira ya saa
mbili asbuhi walikua shambani kuendelea na kilimo,
ghafla walisikia
sauti ya mtoto akilia kichakani na walipofika walimuona mtoto akiwa
ndani ya mfuko wa saruji ndani yake mukiwa na makumbi pamoja na nguo
chafu ambazo alizongwa nazo.
“wakati tunaendelea kulima mimi na mke wangu tukasikia sauti ya mtoto
kwa ikiliya, tukatafuta hatimae tukaona mfuko wa saruji ambapo
tuligundua kuwa sauti ya mtoto huyo ndimo inamotokea, baada ya kuufungua
tukamuona mtoto akitokwa na mafunza mdomoni na kituvuni”alisema Kombo.
Kombo aliendelea kueleza, mara baada ya kuona hali hiyo walimchukua
mtoto huyo mpaka kwa sheha wa shehia hiyo ndg: Rehema Abdalla Omar
ambapo kwa kushirikiana na wanakijiji wengine walimuwahisha katika
hospitali ya Wete ili kupatiwa huduma ya kwanza na kuyanusuru maisha
yake.
Kwa upande wake Muuguzi wa wodi ya watoto katika hospitali ya Wete
Bahati Ali alikiri kumpokea mtoto wa siku tatu aliyeletwa katika
mazingira ya kuokotwa, alisema baada ya kumpokea alimpatia huduma.”
alikua na kilo 3.1 na anaonekana kuwa alizaliwa akiwa na afya nzuri ”
alisema Ali
Uchunguzi uliyofanywa na Dk Hawala Saleh Mohd kitengo cha uzazi
hospitali ya wete umethibitisha kuwa mama wa mtoto huyo Hadia Ali
Mbarouk alionekana kuwa ni mtu aliyejiufungua siku tatu nyuma.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 35 ambae ni mjane mwenye watoto
watatu mara baada ya kukamatwa alisema kuwa, aliamua kumtelekeza
mwanawe kwakua awali alikemewa sana na mamaake kuwa hataki mtoto wa nje
ya ndoa.
Amesema kwa kumuhofia mamaake na aibu kutoka kwa ndugu jamaa na
wakaazi wengine wa maeneo hayo aliamua kumtupa mtoto wake ili
kujinusura na janga hilo.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kaskazini Pemba Mlenge Mohd
Mlenge amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa
aliyemtupa mtoto huyo yupo chini ya uwangalizi wa madaktari katika
hospitali ya wete na mara baada ya hali yake kiafya kuwa nzuri hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mpaka sasa mtoto yupo katika hopitali ya Wete anaendelea kupatiwa matibabu na afya yake inaendelea kuwa vizuri.
chanzo:zanzibar24.
Comments