Makaazi 38,000 ya haribika kwa mafuriko nchini China.

Takribani watu 56 wamefariki na wengine 22 hawajulikani waliko kufuatia mvua kubwa zilizopelekea mafuriko makubwa yaliyoharibu miundombinu ya umeme, nyumba na ofisi.

Mafuriko hayo yamepelea mito 60 kujaa kupita kiasi hali iliyosababisha watu zaidi ya Milioni 1.2 kuokolewa baada ya kuzingirwa na maji.


Mamlaka zimesema kuwa makazi 38,000 na hekta 880,000 za mazao zimeharibiwa vibaya. Serikali imetoa Dola za Kimarekani Milioni 103 kwa wakazi hao kama msaada wa dharula.
chanzo: zanzibar24.

Comments