Chadema yalani vitendo vya uhalifu Mkoa wa Pwani Kibiti.

Chama cha Demokrasia na maendeleo chadema  kimelaani  vikali vitendo  vya udhalilishaji unavyoendelea kutokea  ambavyo  hufanyiwa viongozi  na wananchi wasio na hatia  pamoja na mauwaji  yanayofanywa na watu wasio julikana yanayoendeleo mkoa wa pwani.

Akitoa  tamko la chama  kwa waandishi wa habari  la kukemea na kulaani  vitendo hivyo  Mwenyekiti Mkoa wa mjini Magharibi ambae pia ni Mbunge  viti maalum Maryam Salum Msabaha
amesema  vitendo vya  ukatili na udhalilishaji pamoja na vitisho  wanavyofanyiwa viongozi  wa chama chao  ni viashirio vibaya  katika chama  na  kufanya hivyo ni kutaka kuikandamiza  siasa  na kuizoofisha demokrasia.

Akizungumzia mauwaji   ya raia pamoja na askari wa jeshi la polisi katika mkoa wa pwani Kibiti,Rufiji  amesema wanalaani vikali   na kulitaka jeshi la polisi  kuongeza juhudi za kuwasaka wahalifu ili kukomesha kabisa vitendo hivyo na kutoa wito kwa wanasiasa kuwacha  tabia za kuingilia kazi za jeshi hilo katika mapambano hayo ambapo amedaini kufanya hivyo ni kurudiasha nyuma jitihada za polisi kuwakamata  wahalifu hao.

Kwaupande wake  Mwenyekiti  kanda ya Unguja Said Mzee Said akizungumzia kauli iliyotolewa  hivi karibuni  na  Rais wa Jamuhuri ya muungano Tanzania John Pombe Magufuli amesema chama hakikuridhia kauli hiyo  ya kumsitisha mtoto wa kike aliepata ujauzito  kwenda shule ni kumnyima  fursa  na haki yake ya msingi mtoto wa kike ya kupata elimu.

Amesema ipo haja  kwa baadhi ya watoto wakike walio pata ujauzito kwa njia ya ubakaji  kufikiriwa kwa undani zaidi ili kupewa haki yake ya elimu  na  kutoa wito kwa viongozi wenye  dhamana  kuifatilia kiundani kauli  hiyo hususani wadau wa elimu  ili kuwatetea watoto  kurudi skuli kuendelea na elimu.
NA:AMINA ZANZIBAR24

Comments