
Wakati fedha hizo zikiwa mikononi mwa wadaiwa, tayari shilingi
bilioni 2.3 ndizo pekee, zilizokwisharejeshwa na wakopaji, ambapo kati
ya hizo shilingi bilioni 42, shilingi bilioni 7.7 Bodi hiyo ilizirithi
kutoka kwa uliokuwa mfuko wa elimu ya juu Zanzibar, ambao ulikoma
kufanya kazi zake mwaka 2011.
Bodi hiyo ya mikopo ya elimu ya juu, kila mwezi hukusanya wastani wa
shilingi milioni 100, kutoka kwa wakopaji ambao ni wanafunzi kila mwezi
hadi mwezi Juni mwaka huu wa 2017.
Aidha taarifa ya Bodi hiyo inaeleza kuwa, tokea kuanza kwake mwaka
2011, wanafunzi zaidi ya 18,994 waliomba kupatiwa mikopo, ingawa baada
ya kupitia vigezo husika, ni wanafunzi 5, 293 ndio walioteuliwa kwa
kipindi hicho, hadi mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini
Chakechake, Mratibu wa Bodi hiyo, kisiwani Pemba Ahmada Omar Juma kwa
niaba ya Mkurugenzi wake, Idd Khamis Haji, alisema urejeshaji umekuwa wa
kusuasua.
Mkurugenzi Iddi alisema, fedha ambazo ziko mikononi shilingi bilioni
39.7 kwa wanafunzi ambao wameshahitimu bado ni nyingi, hivyo ni lazima
kwa waajiri iwe wa serikali au taasisi binafsi, kufanya uhakiki na
wakiwagundua waliosomeshwa na Bodi hiyo, wasisite kutoa taarifa kwao.
Alieleza kuwa, zipo sheria za Bodi hiyo, ambazo bado hazijatumika
ipasavyo juu ya wanafunzi waliomaliza na kutotoa taarifa za makato,
lakini kama wataendelea kuwa wasugu, zitatumika ikiwa ni pamoja na
kuanza na wadhamini wao.
“Kuna adhabu mpaka shilingi millioni 5,000,000 au kifungo kwa
madhamini, lakini hata kwa mkopaji kutakiwa kulipa deni kwa mkupuo au
kuligawa, endapo kutakuwa na hali ya kukimbia ulipaji wa deni
lake”,alifafanua.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo alisema, changamoto kubwa hasa
inayowakabili, ni pamoja na wale wanaoajiriwa kwenye mashirika binafsi
na kisha waajiri kushindwa kutoa ushirikiano wa dhati na bodi.
Aidha amesema wengine hata kwa mashirika ya umma, wamekuwa wazito
kutoa taarifa za waajiriwa wapya, na wale wanaoondoka nchini kufuata
ajira nje ya nchi.
“Suala la kurejesha mikopo halimuhusu mkopaji pekee, bali hata
muajiri na mdhamini ni lao, maana fedha hizo zinahitajika kuzngurushwa,
ili na wengine wapate kuziomba”,alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Hassan Khamis Hassan kutoka Konde, alisema yeye
alishawahi kumpelekea ripoti mwanafunzi aliemdhamini, ambae kwa sasa
anaendelea kukatwa.
“Nilimuuliza kuwa, umeshaanza mikato, akanionyesha dharau, lakini
baadae nilipomfahamisha alikubali kwenda kujipelekea ripoti na sasa
anaendelea kukatwa”,alisema.
Hata hivyo mwanafunzi Asha Mohamed Ali, alisema lazima fedha za
kujikimu ziongezwe, maana maisha hasa ya chuoni yamekuwa magumu kutokana
na kupanda kwa bei ya vyakula.
Wakati huo huo Mratibu wa Bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kisiwani
Pemba Ahmada Omar Juma, amempongeza rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, kwa kutimiza ahadi yake
ya kuwaongoeza bajeti kwenye bodi yao.
Alisema ongezeko hilo ni kutoka shilingi bilioni 6.8 kwa mwaka
uliomalizika wa fedha 2016/2017 hadi kufikia shilingi bilioni 10.2 kwa
mwaka 2017/2018, jambo ambalo limewapa kufanya kazi zao kwa ufanisi.
“Lazima tumpongeze rais wetu pamoja na waziri na hata baraza la
wawakilishi, kwa kukubali kutuongezea na kupitisha ongezeko la bajeti
kwenye bodi yetu”,alifafanua Mratibu huyo.
chanzo:zanzibar24.
Comments