Amesema kumejitokeza hofu kwa baadhi ya watendaji wa sekta
zilizopeleka madaraka katika serikali za mitaa, kwamba watapoteza
nafasi zao za kazi jambo ambalo sio la kweli.
Akifungua mafunzo kwa watendaji wa vikosi kazi vitano vya
utekelezaji wa malengo ya sera ya ugatuzi, mh. Hijja, amesema
jitihada zinaendelea kufanyika za kutoa elimu kwa kushirikisha
wataalamu ili kuona mpango huo serikali unafanikiwa.
Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji mjumbe wa kikundi kazi
masuala ya fedha, nd. Haji ali haji, amesema wametayarisha mpango
kazi kwa kujifunza kwa baadhi ya nchi zilizopata mafanikio
kupitia ugatuzi.
Mtaalamu ushauri rasilimali watu, richard kimey pamoja
mtaalamu rasilimali fedha, gikene john, wameshauri kuandaliwa
sheria madhubuti na kanuni za kusimamia suala ugatuzi ili
kuepusha migongano ya kiutendaji.
chanzo:Zbc.
Comments