Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 8 mchana huko Kiwambamvua wilaya ya Kaskazini B, mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Sheha wa shehiya ya Kiwambamvua
Moh’d Ali Ame amesema kijana huyo amezama kwa muda mrefu hadi wao
kufikiwa na taarifa hiyo na baada ya kuzipata taarifa hizo aliripoti kwa
Mkuu wa wilaya na vikosi vya Polisi ili kushirikiana kumuokoa kijana
huyo.
Nae Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Unguja bi Asya Ramadhan
Tawfiq amesema marehemu anajulikana kwa jina la Haji Pandu Faki mkaazi
wa Kiwambamvua.
Bi Asya amesema kabla ya kifo chake marehemu alikuwa na wenzake
wakaenda sehemu hiyo kwaajili ya kukoga ndipo maji yalipo mzidi na
kusababisha kifo chake.
Mwili wa marehemu ulipelekwa Hospitali kuu ya Mnazi mmoja kwaajili ya uchunguzi na kukabidhiwa jamaa zake kwa ajili ya Mazishi.
chanzo: zanzibar24.
Comments