Jana
miswada mitatu inayohusu madini ilisomwa bungeni kwa mara ya kwanza
jana. Miswada hiyo iliwasilishwa kwa hati ya dharura kama ambavyo Rais
Magufuli aliliomba Bunge lipitie upya sheria na mikataba ya madini.
Bunge pia limeongezwa muda hadi July 5.
Wakati
anapokea ripoti ya pili ya Kamati Maalumu ya Uchumi na Sheria kuhusu
Taarifa ya Makinikia, Rais Magufuli aliliomba Bunge kupitia upya sheria
na mikataba yote ya madini na gesi ili kuiepusha nchi kuingia katika
mikataba mibovu.
Baada ya kuwasilishwa kwa miswada hiyo jana, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika(Chadema) aliomba mwongozo wa Spika, ambapo aliliomba bunge kuondoa hati ya dharura ya kujadili miswada hiyo.
“Muda
mfupi uliopita tumekabidhiwa ratiba ya bunge, serikali inaleta miswada
mitatu kwa hati ya dharura, mwaka 1997 mikataba ya madini ilipitishwa
haraka haraka, mikataba ya ngesi hivyo hivyo,
“Kazi
ya bunge ni kutunga sheria, sisi ndio wawakilishi wa wananchi, kwa
umuhimu wake na maslahi kwa wananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa
kukutana na wananchi, hivyo ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza na
hati ya dharura ikaondolewa na kuletwa bunge lijalo.
“Kwa
maelezo uliyotoa wadau wataitwa kwa short notice wafike Dodoma
kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichambue.
Huu ni mtego kwa kutufanya tushindwe kuishauri serikali kwa kazi yetu ya
kibunge”. Alisema Mnyika
Baada ya kauli hiyo ya Mnyika aliyoitoa jana Bungeni, leo Zitto Kabwe(Mbunge wa Kigoma-ACT Wazalendo) amepingana na kauli hiyo ambapo amesema Hoja ya hati ya dharura anayoizungumzia Mnyika ni dhaifu kwa sasa.
==>Huu ni ujumbe wake aliouandika kupitia ukurasa wake Facebook
Naelewa
Sana wenzangu wanapoongelea hati ya dharura kwenye miswada Hii ya
Rasilimali za Nchi. Lakini ukisoma muswada mmoja baada ya mmoja hakuna
jambo linalohitaji muda maana yote tumekuwa tukiyasema Kwa miaka 10 sasa
tangu Buzwagi Mwaka 2007. Hoja ya hati ya dharura ni dhaifu Kwa sasa na
Kwa hili.
- Sheria moja inataka tamko rasmi la kisheria kuwa madini, mafuta na gesi asilia ni mali ya Taifa ya milele na haitahamishwa Kwa yeyote. Tukiongezewa muda tutabadili hili?
- Sheria moja inataka mikataba ya Madini iwe inapitishwa na Bunge. Tukiongezewa muda tutabadili hili?
- Sheria moja inabadili sheria ya Madini ya mwaka 2010 Kwa kutekeleza mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Unataka muda Kwenye hili?
Hebu tukatunge sheria na tuboreshe miswada Hii ili kurudisha rasilimali zetu kwenye mikono yetu. Hoja ya Hati ya Dharura ni hoja nzuri lakini Kwa sasa ni maneno matupu yaani empty rhetori.

chanzo:Mpekuziblog.
Comments