Zanzibar ipo hatarini kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi inayojitokeza.

zaccaJumuiya ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ZACCA imesema  visiwa vya
Zanzibar vinakabiliwa na mabadiliko ya tabia ya nchi yatayosababisha upoteaji wa misitu ya asili, kuongezeka kwa maradhi ya miripuko na kupotea kwa rasilimali ya mchanga.

Akizungumza na  Waandishi wa habari  ikiwa ni  shamrashamra ya kuadhimisha  Siku ya mazingira duniani  ambayo inatarajiwa kuadhimisha tarehe 5  huko Musoma Butiama Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Amina Yussuf Kashoro amesema  uharibifu wa mazingira  unapelekea  kuongeza kasi  ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo uchimbaji mchanga,
ukataji misitu kwa matumizi ya mkaa na kuni, uharibifu wa vyanzo vya maji ikiwemo ujenzi na ulimaji katika maeneo ya vyanzo vya maji na kusababisha mafuriko.

Hata hivyo Amina amesema licha yajuhudi mbalimbali  zinazochukuliwa kupambana na matatizo lakini bado  yanashika kasi  na kuhatarisha mustakabali wa zanzibar kimazingira  hivyo  niwakati muafaka  kwa jamii kuwa na uelewa juu ya tatizo hilo na kutafuta njia bora  za kilimo na ufugaji kwani mabadiliko hayo  yameathiri sana mifumo ya maisha ikiwemo kilimo,ufugaji,nishati,utalii pamoja na afya.

Aidha Zacca  imeishauri Wizara ya fedha kutenga  fedha zaidi kusaidi miradi ya jamii  ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi ili kupunguza kasi kwa jamii kuharibu mazingira kama ukataji miti ovyoo kwaajili ya mahitaji yao.

Amesema ipo haja serikali  kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo  kuweka nguvu zao katika kuwaelimisha jamii juu ya athari hizo kwani tafiti zilizofavywa na idara ya misitu na maliasili zisizorejesheka inaonesha  zanizbar inapoteza hekta 500 kwa kila mwaka kutokana  wananchi wa Zanzibar wanategemea  kuni na mkaa kwa asilimia 97.
chanzo: Zanzibar24

Comments