
Akizungumza baada ya kuitembelea Skuli hiyo na kusikiliza maelezo
kutoka kwa walimu, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Riziki Pembe Juma amelaani
vikali kitendo hicho, amesema Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11
amefanyiwa ukatili mkubwa kwa kupewa adhabu isiyoendana na umri wake.
Nae Waziri wa kazi, uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto
Mhe. Maudline Cyrus Castico amesema kitendo alichokifanya Mwalim huyo
kwa kumpiga na kumuumiza marehemu ni udhalilishaji na kuvitaka vyombo
husika kuchukua hatua za kisheria dhidi yake.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Sheikhan
Mohammed Sheikhan amesema tayari jalada la kesi hiyo limeshafunguliwa
ingawa upelelezi bado haujakamilika.
chanzo: zanzibar24.
Comments