
Akiwasilisha hutuba ya makadirio ya Mapato na matumizi ya Fedha ya
mwaka 2017/18 katika kikao cha Baraza la wawakilishi chukwani Nje kidogo
ya mji wa Zanzibar ,Waziri wa Afya Mahmod thabit Kombo amesema yapo
majengo makuu matatu ambayo ni chakavu kutokana na kutumika kwa muda
mrefu.
Amesema miongoni mwa majengo hayo ni pamoja na jengo la hospitali ya
Mnazi mmoja ambalo limedumu kwa miaka 94 tangu kuanzishwa kwake,Jengo la
hospital ya magonjwa ya akili lililodumu kwa kipindi cha miaka 68
pamoja na kuchakaa kwa Paa la Hospitali ya chakechake.
Aidha amesema mbali na tatizo hilo wizara ya afya imekabiliwa na
tatizo la kuengezeka kwa mahitaji ya huduma za afya wanazohitaji
kupatiwa wagonjwa licha ya kutengewa bajeti na serikali.
Akizungumzia suala la kupandisha hadhi hospitali Kuu ya Mnazi mmoja
Waziri kombo amesema katika mwaka 2017/18 wizara imekusudia kuengeza
upatikanaji wa vifaa tiba ,kuendeleza ujenzi wa wodi mpya ya watoto
inayotarajiwa kuwa na vitanda100 pamoja na kulikarabati jengo la macho
lililopo katika hospital hiyo ili kutowa huduma bora kwa wagonjwa.
Hata hivyo amesema wizara pia imenunua mashine itanayowasaidia
wagonjwa wa matatizo ya figo (dialysis ) kuweza kusafisha damu, pamoja
na kuimarisha huduma za uchunguzi ikiwemo huduma za X-RAY, MRI na
ULTRASOUND.
chanzo: Zanzibar24.
Comments