
Wengi wa waliofariki inaaminika wamefariki kutokana na kukosa hewa
safi kutokana na moshi uliotanda mwanamume huyo alipowasha moto meza za
chumba hicho cha kamari.
Mwanamume huyo alianza kwa kupiga risasi skrini za TV katika chumba hicho cha Resorts World Manila mapema Ijumaa.
Maafisa awali walisema hakuna aliyekwua ameumia kutokana na kisa
hicho, lakini sasa inabainika kwamba wamepataa miili ya watu wakikagua
chumba hicho.
Polisi wanasema kisa hicho kinaonekana kuwa kisa cha kawaida tu cha wizi, na kwamba hakikuhusiana na ugaidi.
Watu zaidi ya 50 wamepelekewa hospitalini wakiuguza majeraha.

Comments