Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka watendaji wa baraza la vijana Zanzibar kuwa na mashirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi katika baraza na kuwacha tabia ya kujigawa matabaka jambo litalopelekea kuvuruga umoja wao wa kuliletea taifa maendeleo.
Akizungumza katika mkutano na baraza la vijana wa kupitisha mikakati na kanuni za baraza zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku amesema ili baraza liwe imara lazima watendaji kupitisha mikakati imara pamoja na kanuni itakayowasaidia kujenga na kuimarisha maendeleo ya vijana na taifa zima.
Hata hivyo amesema Serikali inalengo la kuwawezesha vijana kiuchumi ili kuweza kujikwamua na hali ngumu ya maisha kwa kutumia fursa zilizopo ambapo lazima vijana kuwa na moyo wa kizalendo wa kujitolea katika kupeleka mbele maendeleo ya taifa.
Kwaupande wake Katibu Mtendaji wa baraza hilo Khamis Faraji Abdalla Akizungumza na mwandishi wetu nje ya mkutano huo amesema mpango huo wa kupitia na kupitisha mpango mkakati wa baraza la vijana na kupitisha kanuni za uongozi na utawala utawasaidia viongozi jinsi ya kuyaongoza mabaraza ya vijana kwa mujibu wa kisheria na kanuni za kiuwendeshaji wa mabaraza hayo.
Mkutano huo wa baraza la vijana ni wapili kufanyika zanzibar.
chanzo:zanzibar24.
Comments