Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameitaka serikali ya Mapinduzi
kuwa makini wakati wa kufunga mikataba ya ujenzi wa majumba na
wakandarasi ili kuepusha hasara kwa serikali na kuepukana na majengo
yasiyokuwa na viwango na ubora ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya
wananchi.
Wakizungumza katika Kikao cha baraza la Wawakilishi Ali Salum
Haji,Miraji Khamis Kwanza na Sheha Hamad Matar
wamesme kutokana na
matatizo na kasoro mbalimbali zilizojitokeza kutokana majengo yasiyo na
viwango yaliyojengwa na wakandarasi ni mabovu licha ya serikali kutoa
mabillion ya Fedha yameweza kusababisha hasara yakiwemo majengo ya
skuli kuvuja, majengo ya wizara pamoja na nyumba za viongozi pamoja na
nyumba za maendeleo wanazoishi wananchi maeneo mbalimbali.
Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said amesema Serikali
imekuwa inaingia katika mikataba ya ujenzi kwa wakandarasi ambao
wanafani na kazi hiyo kwa mujibu wa sheria na sifa za kuingia kwenye
mkataba lakini chanzo cha majengo hayo kutokuwa na ubora na viwango
ni usimamizi mbovu wa mikataba hiyo pamoja na watendaji wa serikali
kutokuwa na udhati wa kufatilia shughuli za serikali.
Kwaupande wake Naibu Waziri wa wizara hiyo Mohammed Ahmada Salum
amesema katika mwaka wa Fedha 2017/2018 serikali itahakikisha
kuyafanyika kazi matatizo yote yaliyojitokeza ili yasijirejee tena
kutokana na hasara kubwa ilopatikana kwani majengo mengi ni mabovu hivi
sasa ili kuhakikisha mikataba inayofungwa na serikali na wakandarasi
inasimamiwa ipasavyo.
chanzo: Zanzibar24
Comments