Uongozi wa TAYI walia na vijana wa kikwajuni.

tayiUongozi wa kituo cha  maendeleo ya vijana  Tanzinia Youth Ico (TAYI) umesema unasikitishwa sana na baadhi ya vijana  wa maeneo ya kikwajuni kufanya  vitendo vya  hujuma  na wizi katika kituo hicho hali ambayo  inarudisha nyuma maendeleo ya  kituo hicho.

Akizungumza na waandishi Mwenyekiti  mtendaji  kutoka tay  Abdalla Miraji Othman amesema kituo  hicho kinawasaidia vijana katika mambo  mbalimbali ya ujasiriamali na elimu ya ukimwi lakini  jambo lililowavunja moyo  nipale vijana wa maeneo hayo kufanya vitendo vya wizi kwa kuiba TV mbili, Dishi, Friji  na mambo mengine.


Hata hivyo amesema lengo la kuanzishwa kituo hicho ni kuwasaidia  vijana wa jimbo la kikwajuni kuweza kupata elimu  ya kujiendeleza lakini  lengo hilo bado halijafikiwa  kwani  mtazamo wao umeenda kinyume kwa vijana hao  na badala yake  kituo hicho kinawafaidisha  vijana wengine mbali na kikwajuni.

Aidha  mwenyekiti ametoa wito  kwa wazazi na walenzi   wa jimbo la kikwajuni kuwanasihi watoto wao kukitumia kituo hicho ili   kuweza kufaidika  na elimu zinazotolewa katika kituo hicho.
chanzo: zanzibar24.

Comments