
Amesema mkataba huo si wa haki na unahatarisha mamilioni ya nafasi za kazi za watu wa Marekani.
Kujitoa katika mkataba huo ilikua ni mojawapo ya ajenda wakati wa kampeni za Trump.
Bw
Trump amesema yuko tayari kuanzisha mashauriano ya mkataba mpya au
airejeshe Marekani baadaye katika mkataba huo chini ya masharti
yaliyoimarishwa.
Lakini amesema kuwa yeye hawezi kuunga mkono
makubaliano ambayo - kwa matamshi yake mwenyewe - yanaadhibu Marekani
bila kuwawajibisha wachafuzi wakubwa wa mazingira, ambapo amezitaja
China na India.
Bw Trump amesema wakati wa kampeni za urais mwaka
jana, aliahidi kwamba angechukua hatua kusaidia sekta za mafuta na makaa
yam awe nchini Marekani.
Wapinzani wake wanasema kujiondoa kwenye
Mkataba huo ni sawa na Marekani kuyakimbia majukumu yake kama kiongozi
katika kukabili changamoto hiyo inayoikabili dunia.
Mkataba wa
Paris unaitaka Marekani na nchi nyingine 187 kudhibiti ongezeko la
viwango vya joto duniani kuhakikisha kiwango cha joto kinafikia
nyuzijoto 2C chini ya kiwango kilichokuwepo kabla ya mageuzi ya
kiviwanda, na baadaye kukipunguza zaidi hadi nyuzijoto 1.5C.
Ni Syria na Nicaragua pekee ambazo zilikataa kutia saini mkataba huo.
Akihutubu
katika bustani ya White House Rose, Bw Trump amesema mkataba huo wa
Paris unalenya kuidhoofisha na kuifanya Marekani kuwa nchi maskini.
Amedai
mkataba huo utaigharimu Marekani $3tn ya mapato na nafazi za kazi 6.5
milioni - huku mataifa yanayoshindana na Marekani kama vile China na
India yakifaidi.
"Ili kutimiza wajibu wangu wa kuilinda Marekani
na raia wake, Marekani itajiondoa kutoka kwa Mkataba wa tabia nchi wa
Paris ….lakini itaanza mashauriano ya kujiunga tena na mkataba huo wa
Paris au mkataba mwingine mpya kabisa kwa masharti ambayo ni nafuu kwa
Marekani," alisema.
Kwenye hotuba yake, alikariri baadhi ya maneno aliyokuwa akiyasema kwenye kampeni.
"Hatutaki viongozi wengine na nchi nyingine ziwe zinatucheka tena - hilo halitafanyika," alisema.
"Nilichaguliwa
kuwawakilisha raia wa Pittsburgh, na si wa Paris.
Niliahidi ningejitoa
au kushauriana upya kuhusu mkataba wowote ambao haujali maslahi ya
Marekani. Mikataba mingi ya kibiashara itaanza kujadiliwa upya
karibuni."
Mwandishi
wa BBC Rajini Vaidyanathan mjini Washington anasema hatua hiyo ya Bw
Trump itashangiliwa sana na wengi wa wafuasi wake, wengi ambao hawajali
sana kuhusu sayansi na mazingira.
Wachanganuzi wanasema kujiondoa
kwa Marekani kutoka kwa Mkataba wa Paris kutaifanya vigumu kwa ulimwengu
kutimiza malengo yaliyowekwa katika mkataba huo.
Marekani
huchangia 15% ya gesi kaboni duniani, lakini pia ni mfadhili mkubwa
kifedha na kiteknolojia wa mataifa yanayostawi katika juhudi za mataifa
hayo kukabiliana na ongezeko la joto duniani.
Bw Trump hajasema ni lini hasa Marekani itajitoa kamili kutoka wka
mkataba huo lakini White House ilikuwa imedokeza awali kwamba shughuli
yote inaweza kuchukua hadi miaka minne.

Canada "imesikitishwa sana" na uamuzi huo wa Bw Trump, waziri wa mazingira wan chi hiyo Catherine McKenna aliambia wanahabari.
Waziri
Mkuu wa Uingereza Theresa May, pia ameeleza masikitiko yake na
alimwambia Bw Trump kwa njia ya simu kwamba mkataba huo unalinda "ustawi
na usalama wa vizazi vijavyo."
Mataifa ya Ulaya kaskazini - Sweden, Finland, Denmark, Norway, na Iceland - pia yameshutumu hatua hiyo.

Mataifa yenye visiwa vidogo, ambayo huenda vikaangamia
viwango vya joto duniani vikiendelea kuongezeka, vimepinga pia uamuzi wa
Bw Trump.
Mjasiriamali
mwanateknolojia Elon Musk amethibitisha kwamba ameacha majukumu yake
kama mshauri wa Bw Trump, kulalamika kutokana na hatia hiyo.
chanzo:Bbc.
Comments