Tomondo: Mama ntilie waendelea kutoa huduma mchana wa Ramadhani.

Wakaazi wa shehia ya Tomondo wameilalamikia Serikali kufuatia mama ntilie waliopo katika shehia hiyo kupika na kuuza chakula wakati wa mchana katika kipindi hichi cha mwezi mtukufuwa ramadhani.

Wakaazi hao wamesema vijana wengi kutoka maeneo mbalimbali wamekuwa wakifata chakula kwa mama ntilie hao huku wakaazi hao wakiamini kuwa sheha wa shehia hiyo ana  taarifa kamili za tukio hilo.


Nae sheha wa shehia hiyo hakulizungumzia chochote tatizo hilo huku akiwatupia lawama wananchi hao kwa kupeleka taarifa kwa vyombo vya habari badala ya kumpelekea yeye kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Hivyo wananchi hao waliiomba Serikali kuliangalia kwa kina tatizo hilo na kulichukulia hatua kwani linapoteza maadili ya uislam katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
 chanzo:zanzibar24.

Comments