SMZ yajipanga kuvunja skuli ya vikokotoni kwa dhumuni la kujenga maduka ya kisasa.

wawakilishiMakamo wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inachukua maamuzi ya kuibomoa skuli ya Vikokoni kwa ajili ya  kuliendeleza eneo hilo kwa  ujenzi wa Moli  na kuhamishiwa skuli hiyo katika maeneo ya Rahaleo.

Akitoa kauli ya serikali mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi Balozi Iddi amesema kuibomoa skuli hiyo lengo ni   kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya kusoma kwani eneo hilo baada ya kukamilika itakuwa  na vurugu litalosababisha wanafunzi kushindwa kusoma na skuli ya Darajani  kuibadilisha ili iyendane na shughuli za kibiashara zitakazokuwepo  darajani.


Hata hivyo amesema    dhamira ya serikali ni kujenga mji wa Zanzibar   kuwa katika mazingira bora na wenye kuvutia  kimaendeleo ili kukuza uchumi  wan chi.

Kwaupande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa,Serikali za mitaa na Idara maalumu za SMZ Haji Omar Kheri akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa  Serikali imefanya utafiti wa kina na  wataalamu wote wa mji mkongwe,wamipango miji,wamazingira na wamanispaa  na kuamulika  kuvunja skuli ya vikokotoni na kupafanya eneo hilo kuwa shoping moli na mambo yote yamezingatiwa yakiweno ya  kimazingira,kihistoria lengo ni kuleta maendeleo Zanzibar.
chanzo: zanzibar24.

Comments