
Akisoma taarifa ya kamati ya Bajeti,kuhusu makadirio ya mapato na
Matumizi ya bajeti ya serikali ,muelekeo wa uchumi na mapango wa
maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati
hiyo katika kikao cha Baraza la wawakilishi Chukwani.
Mjumbe wa kamati hiyo Abdallah Ali Kombo amesema mfumko wa Bei
Zanzibar umepanda hadi kufikia asilimia 6.7 mwaka 2016,kutoka asilimia
5.7 kwa mwaka 2015 kutokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula
siku hadi siku.
Amesema Zanzibar ikijitahidi kuimarisha uzalishaji wa ndani
itapunguza kuagiza vyakula kutoka Tanzania Bara na nje ya Nchi na hivyo
kusaidia kuwapunguzia wananchi usumbufu wanaoupata wakati wakihitaji
huduma muhimu za chakula hususani katika kipindi hichi cha mwezi wa
Ramadhani.
Akizungumzia suala la misamaha ya kodi kwa wafanya biashara kamati
hiyo imeomba serikali kuwafatilia ili kuwachukulia hatua wafanya
biashara waliopewa misamaha hiyo na kushindwa kuitumia kwa kutoa huduma
nafuu kwa wanunuzi wao wakiwemo wananchi wa kipato cha chini.
Amesema mbali na serikali kuzisamehe Fedha nyingi za kodi
zilizokusudiwa kukusanywa ili kuimarisha maendeleo ya nchi ,lakini
imeonekana fedha hizo kuwanufaisha Wafanya biashara peke yao,kinyume na
matarajio yaliokusudiwa ikiwemo kupunguza bei kubwa ya bidhaa zao kwa
wananchi wa kipato cha chini.
chanzo:Zanzibar24.
Comments