
Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Naibu Waziri wa
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na usafirishaji, Mhe. Mohammed Ahmada
Salum amesema kulingana na muongozo wa mwaka 1983 ni watu tisa tu
wanaopaswa kulipwa fidia.
Na amefahamisha kuwa mwaka hatua hiyo
inatokana na 1983 Serikali kuweka michoro maalum kuonesha eneo la
hifadhi ya barabara.
Hivyo amesema Serikali haitowalipa wananchi waliojenga kinyume na
taratibu na waliopewa hati ya muda kwa makubaliano ya kuendesha shughuli
zao za biashara katika maeneo hayo ya Serikali.
chanzo: zanzibar24.
Comments