Rais John Magufuli amesema taasisi yoyote ambayo haitalipa bili za maji, hata kama ni Ikulu ikatiwe maji.
Aliyasema
hayo jana Jumatano katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na
kusisitiza kuwa miradi ya maji na ulipaji wa bili za maji ni muhimu.
“Mtu asipolipa bili, iwe taasisi yoyote hata kama ni Ikulu, narudia kusema kata,” alisema na kuongeza:
“Kwa
sababu tumezoa kudekezana, kwenye mawizara haya nafahamu, fedha za OC
na hata fedha za bajeti wanazo, lakini suala la bili ya maji linakuwa si
la lazima.”
Alisema
unamkuta kiongozi ana faili la kwenda Ulaya, anaenda kwanza Ulaya, ana
semina analipa kwanza semina maji anaona si lazima.
“Lakini pale hakuna maji, na wale hawajalipia bili, kwa hiyo fundisho la hapa ni kukata,” alisema.
Alisema hata kama ni hospitali wakatiwe kama hawajalipa kwa sababu wana bajeti.
Alisema kama Mkurugenzi wa wilaya yupo na maji yamekatwa, basi hafai kuwa mkurugenzi.
“ Tukifukuza wakurugenzi kama 10, 20 hivi wale wengine watawahi kwenda kulipa bili za maji,” alisema.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments