Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana
tarehe 21 Juni, 2017 amefuturisha wananchi wa mkoa wa Pwani na kuwataka
waumini wa dini ya Kiislam na madhehebu mengine kuendeleza umoja na
mshikano uliopo kwa muda mrefu kwa lengo la kudumisha amani nchini.
Mhe.
Rais Magufuli alisema anaungana na waumini wa dini ya Kiislamu nchini
katika kumi la mwisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuwaombea
kumaliza kwa amani ibada ya Funga ya Ramadhani ikiwa ni kutekeleza nguzo
ya nne kati ya nguzo tano ya dini ya kiislam.
Alisema
kwa mujibu wa dini ya Kiislamu ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani ni muhimu kwani ni njia sahihi ya kujirekebisha kuachana na
matendo maovu yanayoweza kusababisha kutenda dhambi.
‘’Ramadhani
ni ibada muhimu kwa Waislaam kwani ndio mwezi ambao huchoma dhambi zao
na kutenda matendo mema hivyo ni muhimu kwa ndugu Waislaam kuendeleza
yote mema ambayo wanafanya katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani
ikiwa ni pamoja na kuliombea Taifa.’’
Kwa
upande wake Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakar Zubeir Ali alitaka
wananchi wa Tanzania bila kujali itikadi za kidini kuendelea kuliombea
Taifa ili lizidi kuendelea kuwa na amani.
Nae
Kaimu Sheikh wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamisi Mtupa alimshukuru Rais
Magufuli kwa ukarimu wake wa kuwaaandalia futari wananchi wa mkoa wa
Pwani ikiwa ni pamoja na makundi maalum ya watoto yatima wa kituo cha
Bulome Foundation cha mjini Kibaha mkoani Pwani.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kibaha, Pwani
chanzo:Mpekuziblog.
Comments