
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma
Majid Abdalla, kwenye hutuba yake iliosomwa kwa niaba yake na Katiba
Tawala wa Mkoa huo Yussuf Mohamed Ali, mara baada ya kumalizika kwa
futari ya pamoja ilioandaliwa na NMB.
Mkuu huyo wa Mkoa, alisema inawezekana wapo wateja wenye imani ya
dini ya kiislamu na wengine, wanataka kuingia ndani ya benki hiyo,
lakini wanashindwa kwa kuogopa riba, kwenye mchakato wao wa kujiinua
kiuchumi.
Hivyo, alisema kama uongozi wa NMB, utaanzisha huduma hizo, inaweza
kuwa sababu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ndani ya benki hiyo,
sambamba na pato la taifa kukua kila mwaka.
Aidha Mwanajuma alisema, tafiti mbali mbali zinaonyesha kuwa, iwapo
taasisi za kifedha zitajenga wigo wa kuwa na dirisha linalotoa huduma za
fedha kama mikopo bila ya kuwepo kwa riba, maendeleo zaidi
yatapatikana.
“NMB ni chachu ya maendeleo ndani taifa la Tanzania, lakini kama
mkianzisha na huduma za kibenki zenye mtazamo wa kiislamu, naamini pato
la wateja wenu na la taifa litazidi kupaa”,alifafanua.
Katika hatua nyengine, Mkuu huyo wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma
Majid Abdalla, alisema mpango wa NMB kukutana na wateja wao hasa kwenye
mkusanyiko wa futari ya pamoja, ni jambo jema linalofaa kuigwa na
taasisi nyengine.
“Mkusanyiko huu ni ishara kwamba NMB bila ya kujali itikadi za dini
za wateja wao, imekua karibu nao mno jambo ambalo linaamsha ari na nguvu
kwa uongozi na watendaji, kutoa huduma bora”,alieleza.
Mapema Mkuu wa kitengo cha Huduma Binafsi za wateja na biashara wa
NMB Tanzania Omar Mtiga, alisema NMB imekuwa na utaratibu wa kufutari
pamoja na wateja wake, kama njia ya kukutana nao.
“Tayari tumeshafutari pamoja na wateja wetu wa Dar- es Salaam,
Unguja, Pemba na kisha Mbeya, Mtwara na mikoa mengine ili kuhakikisha
tunakuwa nao pamoja”,alifafanua.
Kwa upande wake Naibu Mufti wa Zanzibar Sheikh Mahamoud Mussa Mawadi,
alisema njia ya kufutarishana ni miongoni mwa ibada moja kubwa, hivyo
mwenendo kama uliofanya na NMB, uingwe na kila mmoja kwa uwezo wake.
NMB kwa upande wa tawi la kisiwani Pemba, limeshatimiza umri wa miaka
20 sasa, ambapo inaowateja zaidi ya 2000 na ATM tatu ambapo makao makuu
yake yapo mjini Chakechake.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments