
Lakini msemo huu unatafsiriwa vizuri hapa Zanzibar ambapo vijana
zaidi 70 wamewezeshwa ili kupata muelekeo kuwa wazalishaji wazuri kwa
ajili ya maendeleo ya Taifa na familia zao.
Vijana hao ambao awali walikuwa wamekata tamaa kwa kukosa jambo la
kufanya ili kujikwamua kimaisha walitafutwa kwa njia mbali mbali ili
kupewa elimu ya uzalishaji wa aina mbali mbalin ikiwemo Kilimo hai
(kilimo asili) ambacho hakitumii kemikali, ufugaji wa Nyuki pamoja
mbolea ya kiasili mradi ambao unajuilikana kwa jina la Fursa kijani.
Mafunzo hayo ambayo yanatolewa yanakuwa na lengo la kuwashajihisha
vijana kujishughulisha na kilimo hai (Kilimo asili) na kuacha
kujishughulisha na kilimo cha kisasa ambacho kinatumia mbolea za
kemikali kwa madai ya kuwa kinaharibu Mazingira na Afya za Binaadamu.
Bernadette Kirsch ambaye ni Muanzilishi wa Practical
Permaculture Institute ya Zanzibar ambayo inawasomesha vijana hao kwa
udhamini wa taasisi ya milele Foundation Zanzibar alieleza kuwa wanataka
kujikita katika kuleta matokeo mazuri yenye faida kiuchumi, kijamii na
kimazingira.
![]() |
Alieleza kuwa vijana wakishapata elimu hiyo wanaombwa kuwasaidia
wengine ili waweze kujikwamua kimaisha kupitia mradi huo Fursa Kijani.
Milele Foundation Zanzibar kwa sasa ndio inayofadhili mradi wa “Fursa
Kijani” ambao ulizinduliwa mwaka 2016 kutengeneza fursa kwa vijana
wavulana na wasichana ”ambao hawapo mashuleni” Kupitia kazi za kijani
wanapata uwezo na ujuzi wa vitendo na pia kuunganishwa na wanufaikaji wa
mradi na ujuzi halisi wa kazi.
Akizungumza na Tanzania daima Mratibu wa Mradi kupitia taaisisi ya
Milele Foundation Zanzibar Bi Khadija Shariff alisema kuwa Vijana hao
hupata ufadhili wa kila kitu kwa wiki mbili ambao unawasiadia kulala
hapo hapo kwenye eneo la mafunzo.
“Lengo kutoa Full scholarship ni kutaka tuwawezesha vijana kikamilifu
ili waweze kutoka na kitu ambacho tumekikusudia kwa ajili yao na nchi
yao” alieelza Bi Hadija.
Alieleza kuwa mradi huo ni wamajaribio ambao ukifanikiwa unalengo la
kuwachukua vijana wengi wazanzibar ili kujenga taifa lenye vijana imara
na maisha bora.
“Tunataka tutoe timu bora ambayo itapelekea kupata na jimii iliyo imara” alieleza Khadija Shariff.
Alifahamisha kwamba Mafunzo yanajumlisha wiki mbili za kujifunza
mambo mbali mbali ikiwemo kilimo endelevu, miezi mitatu ya kujifunza
kazini katika kituo cha Fumba Town Service Center (FTSC).
Licha ya kazi hiyo Milele inaeleza jinsi ilivyopata changamoto kwa
mwaka wa mwanzo ambapo baadhi ya vijana walikimbia kabla ya masomo
kwisha.
“Lakini tuligundua wale vijana walikuwa na shghuli nyengine ndio
ikawa hawakuwa na kitulizano pale chuoni lakini kwa sasa tumejipanga
vizuri” alieleza Khadija.
Alieleza changamoto nyengine ambayo wanakabiliana nayo ni kutokana
kuwa vijana wanawachukua ni kutoka katika familia masikini sana na sasa
wanategemea kila kitu kwao wao na kudai lakini na wao wamejitahidi
kuzitatua na sasa halin inakwenda vyema.
Kituo hicho FTSC kimeonekana kutoa mchango mkubwa kwa vijana hao
kwani mara wanapoamaliza mafunzo kutoka katika chuo cha Practical
Permaculture Institute of Zanzibar huwachukua wahitimu hao na kuwapati
mafunzo kwa vitendo kwa muda wa miezi mitatu.
Mara baada ya kumaliza mafunzo hayo ya vitendo huwafanyia usaili
wahitimu hao na baadae huto ajira kwa wale ambao watafaulu usaili huo
ambapo kwa sasa tayari imeshaajiri vijana 30 kutoka kwenye mradi wa
Fursa kijani kati ya wale zaidi 70 na wengine wamepata ajira kutoka
sehemu nyingine kama vile mahoteli.
Akizungumza na muandishi wa habari hizi huko afisini kwake Fumba nje
ya mji wa Zanzibar ambao una umbali wa karibuni kilo mita 25 kutoka
mjiku wa Zanzibar Mkuruegenzi Mtendaji Sebastian Dietzold alieleza kuwa
lengo lao kuwachukua vijana hao ni kutaka kufikia malengo ya taasisi
yake ya kujenga Nyumba bora.
“Sisi tunajenga nyumba ambayo yatakuwa ni makazi bora , lakini kama
hakuna maisha mazuri, lile lengo tumefikia hamna” alieleza Dietzold.
![]() |
Alieleza kuwa wanawawezesha vijana hao ili maisha yao yawe ya kisasa
ambayo yatategemea zaidi kilimo hai (Kilimo Asili) ambacho hakina athari
kwa binaadamu.
Alieleza kuwa licha ya vijana wengi awali walikuwa hawana uwezo wala
fikra zozote zile, na kueleza kuwa katika taasisi yake anajivunia vijana
wengi ambao wamepata masomo hayo na kuzalisha vitu vya aina tofauti.
“Nawaomba vijana wote ambao hawana uwezo wajitokeze na watawezeshwa
ili na wao waweze kujikwamua kwani fursa zipo nyingi hasa wakishapata
ujuzi” alieleza Dietzold.
Muharami Ali Hamad ni miongoni mwa vijana ambao walipata mafunzo hayo
kupitia mradi huo wa Fursa kijani ambapo leyo anazishukuru taasisi hizo
hasa akieleza thamani yake kubwa kwa Milele Foundation Zanzibar ambayo
ndiyo iliyomdhamini kupata ujunzi ambao anao.
“Leo unapo niona hapa kakaangu nafanya kitu ambacho katika akili
yangu kawaida hakikuwemo namshukuru mola wangu halafu sasa
nisipoishukuru taasisi hii nitakosa radhi zake” alieleza Hamad.
Hamadi ambaye anafanyakazi katika kituo cha Fumba Town Service Center
kitengo chake ni kufuga Asali ya kisasa ambayo inatumia utaalamu wa
hali ya juu tofauti na ile iliozoeleka.
Kwa upande wake Bi Ujudi Ali Khamis ambaye yeye anafanyakazi katika
kituo cha kutengeza mbolea hai ( mbolea Asili) alieleza kuwa ni wakati
wake sasa kuwapitia wanawake wenzake na kuwashawishi waweze kujiunga na
chuo ili baadae waweze kuwa na taifa ambalo vijana waliowengi wanaweze
kujitegemea.
Alieleza kwa sasa kazi yake katika taasisi hiyo ni kutengeza mbolea
na kueleza anapotoka kazini hua anatoa elimu kwa wenzake mitaani .
Akieleza Mkurugenzi wa maendeleo ya Vijana kupitia Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Mwanaidi Muhamed Khamis aliwashauri vijana
hao kuyatumia vyema mafunzo hayo kwa kile alichodai kuwa furaha ya SMZ
ni kuonan vujana wanapata maisha yaliobora kwa ajili ya maendeleo ya
taifa.
Haya ni maendeleo makubwa katika taifa kupitia fikra hii ambayo
ilibuniwa na taasisi hizo tatu ambapo kama jamii itaitumia vile ilivyo
ndivyo basi vijana wengin watakuwa watalamu wa uzalishaji wa vitu mbali
mbali.
Jamii inatakiwa kuchua hii ni fursa adimu ambayo ni ngumu kupatikana
na hivyo kuacha kuingiza siasa na kuchukua wale walengwa waliokusudiwa.
chanzo:zanzibar24.
Comments