
Akijibu swali katika kikao cha baraza la wawakilishi Naibu Waziri wa
Afya Harusi Said Suleiman amesema kuna ongezeko kubwa la ajali za
barabarani zinazosababisha vifo, ulemavu na hata majeraha makubwa jambo
linalohatarisha maisha ya wananchi.
Aidha amesema ongezeko hilo la ajali linapelekea kuongezeka kwa
mahitaji ya huduma za uchunguzi na matibabu ambapo wizara inakabiliwa
na tatizo la uhaba wa madaktari bingwa wa mifupa katika hospitali kuu
ya Mnazi mmoja.
Harusi amesema kitengo cha mifupa hivi sasa kinauhaba wa madaktari
bigwa ambapo kwa sasa kina madaktari wawili, mmoja mzalendo na
mwengine mgeni nakwamba wawili wapo masomoni.
Aidha amesema wizara yake inaendelea na juhudi za kuhakikisha
kitengo hicho kinapata madaktari na wahudumu wenye ujuzi wa kutosha
ili kukidhi mahitaji yaliyopo.
chanzo: zanzibar24.
Comments