
Mzee Ndesamburo amefariki dunia wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Lowassa ameandika, “Nimesikitishwa
sana na kifo cha ghafla cha Mzee Ndesamburo, Mungu ailaze roho yake
mahala pema peponi natoa pole kwa familia na wote.
Mzee Ndesamburo
alikua shujaa wa kweli wa mabadiliko wa miaka mingi na mwenye mchango
mkubwa kwenye siasa za demokrasia katika Taifa letu.

Comments