Jumuiya ya Kutetea Taifa la Palestina imetangaza kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya Uislamu na siku kudhihirisha nguvu ya Umma wa Kiislamu na kuinua juu sauti ya kudhulumiwa.
Taarifa iliyotolewa leo na Jumuiya ya Kutetea Taifa la Palestina imesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds inatoa bishara njema ya kukombolewa wanadamu kutoka kwenye ukoloni wa Uzayuni wa kimataifa na ubeberu wa dunia.
Taaifa hiyo imeongeza kuwa: Utawala habithi wa Israel ndio chanzo cha vita, ukosefu wa amani na kubakia nyuma kunakoshuhudiwa katika eneo la Mashariki ya Kati na kwamba mataifa ya Kiislamu yanalipa gharama kubwa kutokana na kuendelea kuwepo utawala huo.
Taarifa hiyo imesema kuwa, mataifa ya Waislamu yanapaswa kuwa macho na makini mbele ya njama za tawala zilizobakia nyuma za Kiarabu zilizoonesha usaliti wao kwa taifa la Palestina na ambazo zimeziarifisha nchi za Kiislamu na makundi yanayopambana na Wazayuni kuwa ni maadui.
Taarifa ya Jumuiya ya Kutetea Taifa la Palestina imesema kuwa: Njama za Israel za kuvuruga amani na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi na kiwahabi imeonekana waziwazi na kwamba, kuna udharura wa kuwepo azma na irada ya kweli ya kukabiliana na utawala huo haramu na washirika wake wa kikanda na kimataifa.
Jumuiya ya Kutetea Taifa la Palestina imesisitiza kuwa, inapinga hatua yoyote ya kufanya mapatano na kuutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel na inatilia mkazo udharura wa kudumishwa mapambano dhidi ya Wazayuni maghasibu.
Ijumaa ya kesho tarehe 23 Juni ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani na inasadifiana na Siku ya Kimataifa ya Quds.
chanzo: parstoday.
Comments