
Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati akitoa hoja ya
kuahirisha Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar
lililojadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka
2017/2018 kwenye ukumbi wa Baraza hilo Chukwani nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.
Alisema dhamira ya Serikali kupitia Wizara husika ya Afya ni kutoa
huduma bora yaliyobainishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati
wakichangia Hotuba ya Wizara ya Afya.
Balozi alisema yapo malalamikombali mbali ya kiutendaji hasa katika
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja yaliyojitokeza ambayo huleta kero na
maudhi kwa Wananchi wanaofika kupata huduma za matibabu.
Alitanabahisha wazi kwamba baadhi ya Madaktari wamekuwa na tabia
sugu ya kutotekeleza wajibu na majukumu yao wakati wengine wakipenda
kutumia lugha chafu zinazowavunja moyo wagonjwa.
Alisema hatua hiyo inakera na kuchukiza Wananchi kutokana na kufikia
huduma zinazotolewa kamwe hazilingani na fedha nyingi zinazotolewa na
kugharamiwa na Serikali kwa kila Mwezi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba vipo vifaa
kufanyia uchunguzi kwa wagonjwa ambavyo kufanyiwa hujuma kwa makusudi
ili wahusika wawaelekeze wagonjwa kwenda kwenye Hospitali zao au zile
wanazopewa baghshishi.
Alisema kitendo hicho kisichokubalika si cha haki kufanyiwa wagonjwa
ambao wengi wao ni maskini na baadhi yao hutoka masafa ya mbali kama
Vijijini kufuata huduma za matibabu Hospitali za rufaa.
chanzo:zanzibar24.
Comments