Balozi Seif amtembelea Mh. Samia ofisini kwake Jijini Dar es salaam.

Makamo wa pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo amemtembelea Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ofisini kwake.

Viongozi hao wamekuwa  na Utamaduni wa kawaida wa kukutana katika dhana nzima ya mfumo wa kuhudumia Wananchi  katika utendaji na ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali zote mbili  ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kulia akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo asubuhi Ofisini kwake Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Jijini Dar es salaam.

chanzo:zanzibar24.

Comments