Waandishi wa habari Kisiwani Zanzibar wamesema pindipo Serikali itasimamia ipasavyo Sera na Sheria za vyombo vya Habari zinazowataka wanahabari kuripoti matukio kwa yaliopo itasaidi kuleta maendeleo katika jamii.
Wakizungumza katika siku wa Kilele cha uhuru wa Vyombo vya nchini Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Zanzibar wamesema mbali na kujikita katika kuandika habari za ukweli lakini wanarejeshwa nyuma na baadhi ya taasisi kushindwa kujua umuhimu wao katika jamii.
Waandishi hao wamesema Zanzibar kuna matukio mbali mbali ambayo yakiibuliwa yatakuwa chanzo cha maendeleo kiuchumi lakini wanashindwa kuyaibua kutokana na kupokea vitisho, kutengwa na jamii na kutishiwa kupigwa na Wananchi pamoja na Viongozi wanao guswa na habari hizo.
Siku ya uhuru wa Vyombo vya habari huadhimishwa kila ifikapo Mei3 ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu imebeba ujumbe usemao umakini wa fikra kwa nyakati muhimu ,nafasi ya vyombo vya habari katika kuimarisha jamii zenye Amani,Haki na Ujumuishwaji.
chanzo:Zanzibar24
Comments