Zanzibar ipo katika hatua za mwisho za kukodi meli ya Uvuvi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt Ali Mohammed Shein amesema kuwa mashirikiano ya pamoja na nchi ya Djibouti  yatasaidia  kuimarisha a uchumi wa Zanzibar .

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari huko Uwanja wa Ndege wa Zanzibar  mara tu aliporudi katika ziara yake ya siku tatu nchini Djibouti.


Alisema katika mazungumzo yao  na Rais wa Djibouti Ismail Omari Guelleh ambae alimualika rasmi kutembelea katika nchi yake walikubaliana kushirikiana katika  Mambo saba ya msingi ambayo yatasaidia kuleta maendeleo ya nchi .

Aidha akiyataja maeneo hayo alisema kuwa  watashirikiana katika kuimarisha ujenzi wa Bandari ,ujenzi  wa Miundombinu ya Barabara, Mawasiliano ya simu  na  Biashara za viungo (Space) .

Hata hivyo alisema watashirikiana kudhibiti  suala zima majangili wanaohatarisha usafiri wa abiria na mali zao pamoja na kuimarisha ndege za mizigo ili kuweza kuwapa urahisi wafanyabiasha wa Zanzibar .

Alieleza kuwa katika makubaliano hayo waliweza  kukubaliana mambo mbalimbali ambayo yatailetea ustawi mzuri nchi ya Zanzibar pamoja na kutengeneza mpango kazi katika nchi zote mbili ilikuweza kufanya utekelezaji kwenda sambamba .

Dkt Shein alisema kuwa katika ziara yake hiyo ujumbe ambao aliofatana nao wakiwemo mawaziri waliweza kufanya mazungumzo ya pamoja baina ya mawaziri wa pande zote mbili na kuweza kukubaliana mambo ya msingi ambayo waliyowafikiana kuyashungulikia.

Hata hivyo Nchi ya Djibouti waliimba nchi ya Zanzibar kudumisha mashirikiano ya pamoja kwa viongozi  wa ngazi za juu na ngazi za kati ili waweze kutembeleana na kutaka kupeana msaada wa utaalamu wa suala zima la utalii kwa upande wa Zanzibar .

Dkt shein alisema alitembelea sehemu ya bandari aliona namna ya huduma ambazo zinatolewa ni za utaalamu wa kisasa,pia wameweza kuanzisha shirika la ndege la Djibouti na kuwa na ndege moja kubwa na ndogo ndogo .

Alifahamisha  katika makubaliano yao walikubaliana ndege ya Djibouti ya mizigo ije Zanzibar  ili kuweza kufanya kazi za usafirishaji wa mizigo katika nchi mbili hizo .

Pia Mhe. Rais alisema katika kuimarisha kampuni ya uvuvi  wa Zanzibar  mipango imo katika hatua za mwisho za ukamilishaji  na kunatarajiwa kukodi meli za uvuvi kwa hatua za awali hadi itaponunuliwa rasmi   na meli hizo zitakodiwa kwa bei nafuu na wataalamu ambao wanatajiwa kulijenga sokojipya la samaki ni  Shirika la Misaada ya Kimataifa la Japani (JICA).

Na Khadija Khamis – Maelezo  10/5/2017 .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
chanzo: zanzibar24.

Comments