“Taswira mpya ni kufanya kazi kwa misingi ya utawala bora inayotaka
Serikali hii ya Awamu ya Tano na sio muda mwingi kufikiria vitendo viovu
ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya wananchi wetu,” alisema
Mtazaraki.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha kikao
cha Baraza la Madiwani mwishoni mwa wiki, mwenyekiti huyo alitoa rai
kwa watumishi hao kwamba hivi sasa wanapaswa kubadilika na sio kila siku
wanakuwa ni watu ambao wanafanya makosa kwa makusudi huku wakijiua
kwamba wanaumiza wananchi.
Alisisitiza kuwa yeye na madiwani wenzake wamefikia hatua ya
kuwafukuza kazi watumishi wanne waliobainika kufanya makosa ya uzembe na
ubadhirifu wa mali za umma ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia
kama hiyo.
Vilevile aliwataka pia madiwani wahakikishe wanajitambua
katika nafasi zao walizonazo kwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa
miradi ya maendeleo ya wananchi kwenye maeneo yao ili ijengwe kwa
viwango vinavyokubalika.
Pamoja na mambo mengine, watumishi waliofukuzwa kazi katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuwa ni aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kata
ya Kitura, Daniel Komba aliyefukuzwa kazi kutokana na kufanya matendo
kinyume cha dhamira njema kwa kughushi risiti za marejesho ya fedha Sh
350,000 za michango ya wananchi wa kata hiyo.
Ilibainishwa kuwa fedha
hizo walikuwa wamechanga wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo yao
na kwamba risiti aliyoitumia kukusanyia fedha hizo haikuwa risiti
halali ya serikali.
chanzo:Habarileo.
Comments