
Wakizungumza na kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao wamesema bidhaa zinazotumika kwa futari bado hazinunuliki ukilinganisha na mwezi wa kula mchana hali yanayopelekea kushindwa kumudu harama za manunuzi.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiasha wamekiri kuwa hali ya bei bado ipo juu kutokana na serikali bado haijashusha ushuru licha ya kuwa Rais wa zanzibar Dr.Ali Mohammed Shein kusema serikali itashusha ushuru kwa wafanyabiashara zanzibar ili kuwapa unafuu wanunuzi katika kipindi hichi cha funga.
Bidhaa zilizolalamikiwa kupanda bei katika kipindi hichi ukilinganisha na awali kwa upande wa nafaka ni Sukari ambayo kilo 1900 hadi 2000, Tambi kilo 1800,Unga wa sembe kilo 2000 hadi 2200, Njugu mawe kilo 2800 hadi 3000, Choroko kilo 2600 hadi 2800 na kwaupande wa Matunda nanzi moja 1500 hadi 2000,Muhogo fungu 2000,Majimbi fungu 5000,Ndizi mbivu dole moja 3000 hadi 5000 chana ya pukusa 3000.
Wakizungumzi hali ya usafi wa soko wafanyabiashara hao wamesema bado mazingira ya soko hayarithishi licha ya kuchangia pesa ya ufanyia shughuli hizo kila siku.
chanzo:Zanzibar24
Comments