Akizungumza na
wakulima pamoja na wadau mbali mbali wa zao la karafuu wilayani humo katika
ukumbi wa zstc Benjamen Mkapa Mkuu wa
Mkoa wa Kuskazini Pemaba Mh Omara Khamis Othman amesema neema ya mvua ambayo Allah
ameetuneemesha nivyema kuweza kuitumikia ipasavyo kwalengo la kujiwekea rasilimali
ambazo zitatusaidia hapo baadae.
Amesema wakulima
wa zao la karafuu hawana budi kuunga mkono jitihada za Serekali ya Mapinduzi Zanzibara
ya kuliboresha zao hilo ikiwa ni pamoja na kuongeza vitalu ili kuondoa usumbufu
wa upatikanaji wa miche kwa urahisi zaidi.
Amefahamisha kuwa
katika kuthamini jitihada za serekali ipo haja kwa wakulima na wadau wengine
kushirikiana kulikuza zao la karafuu ili kurejesha hadhi iliyokuwepo awali
isipotee.
Ameeleza kuwa
wakulima kwapamoja nihaki yao kuendelea kuwashukuru viongozi wao kuendelea
kulinda thamani ya bei ya zao hilo isishuke na kuweza kuleta madhara kwa
wananchi pamoja na wadau wengine.
Kupitia mkutano
huo maalum Mkuu huyo wa Mkoa amechukua nafasi ya kutoa mkono wa pole kwa
wananchi wote waliopata madhara yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha kuendelea
kuwa wastahamilivu katika kipindi hichi
kigumu kwao kwani serekali inaendelea kufanya tathmini juu ya wale wote waliopata
majanga hayo na kuendelea kutoa taarifa sehemu husika kadri hali inavyo
endelea.
Comments