Waislam watakiwa kutokubali kuyumbishwa.

Image result for SHEIKH KHALFAN SULEIMAN TIWANIYWaislamu nchi wametakiwa kuwa kitu kimoja na kuacha tabiya ya baadhi watu kuto wayumbisha kwa sababu za madhihebu ya wengine.

Akiwahutubia waumini wa dini ya kiislam katika masjid L-KHALIL uliopo Mtoni Chake Chake kupitia  khutba ya swala ya Ijuma Sheikh Khalfan Suleiman AL-tiwaniy ambae pia ni mmoja kati ya viongozi wa jumuiya ya Istiqama Pemba amesema waislam wasikubali kuchezewa na makundi yasiyo watakia mema katika ibada zao.


Amefahamisha kuwa kila ifikapo mwezi wa Ramadhani huzuka makundi yanayo sambaza taarifa zisizo sahihi nakuwataka waislam kufuata mwandamo wa mwezi kulingana na nchi utakako onekana jambo ambalo amesema sio sahihi.

Ameeleza kuwa makundi ya aina hiyo yanapaswa kujiamulia wenyewe bila ya kuwashirikisha waumini wengine kwani kufanya hivyo kunaleta mgawanyiko  ndani ya dini ya kiislam.

Aidha amewakumbushia waislam  juu ya muda wakula daku nakusema kuwa muda sahihi wa mwisho ni wakati wa kupambazuka kwa Alfajiri.

Amefahamisha kuwa waislam wakumbuke mtu kujitoa shahwa kunasababisha funga yake kupotea hivyo kujiepusha kufanya kitendo hicho nakutupilia mbali kauli za baadhi ya watu wanao dai kuwa hakubatilisha swaumu ya mgafungaji.


Sambamba nahayo amewaomba waislam kufunga na kufungua kulingana na mwendamo wa mwezi na endapo kutajitokeza khitilafu kiongozi mkuu ambae ni Mufty wa nchi kuweza kuweza kuzungumzia tukio hilo.

Comments