
Aidha taarifa hizo zilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa Chama cha
Mapinduzi kipo katika wakati mgumu kuweka wazi kuhusiana na kujiuzulu
kwa Katibu Mkuu huyo.
Habari za uhakika zilizotolewa na Katibu wa Itikadi na uenezi wa
chama hicho Nd. Humphrey Polepole ni kuwa Kinana hajajiuzulu nafasi hiyo
na kwasasa yeye (polepole) pamoja na Kinana wapo nchini Angola
wakipeleka ujumbe wa CCM mpya kwa vyama rafiki.
Polepole aliyasema hayo kupitia kwenye mtandao wa Twitter akimjibu
mmoja wa waliomuuliza kuhusiana na ukweli wa jambo hili “Kazi yao
kuzusha uongo kila siku, mimi, Ndg. Lubinga na Ndg. Kinana tuko Angola
kikazi, huko tumepeleka ujumbe wa CCM mpya kwa vyama rafiki” Aliandika
Polepole
chanzo: zanzibar24.
Comments