
Imesema
kuwa hatua hiyo inafuatia uamuzi wa rais huyo kupiga marufuku mitandao
ya kijamii ya Urusi ambayo ni maarufu sana nchini Ukraine.
Kiev haikutoa ushahidi wowote unaohusisha Urusi na uvamizi huo.
Hatahivyo Urusi haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo ya Ukraine.
Utawala wa rais huyo wa Ukraine umesema kuwa hali hiyo 'imedhibitiwa' na hakuna tishio lolote katika kazi ya tovuti hiyo.
Saa
kadhaa baada taarifa ya utawala huo, tovuti hiyo ilianza kufanya kazi
kama kawaida huku viunganishi vyote vya habari katika ukurasa wa kwanza
vikipatikana.
Uamuzi wa Ukraine kupiga marufuku mitandao hiyo ya
Urusi mapema Jumanne ni mojwapo ya hatua ya kuiwekea vikwazo Urusi kwa
kuiteka Crimea 2014 mbali na madai ya kuhusika na mzozo mashariki mwa
Ukraine.
Mitandao iliolengwa ni pamoja na Vk.com na Odnoklassniki, Mtandao wa kutafuta, Yandex na huduma za barua pepe za Mail.ru.
Kampuni za huduma za mitandao zimeagizwa kufungilia mbali mitandao hiyo.
Mali
zilizopo katika afisi za kampuni hizo nchini Ukraine pia zimepigwa
tanji na kuwekewa vikwazo ijapokuwa haijulikani marufuku ya huduma hizo
itatekelezwa vipi na iwapo Ukraine ina uwezo wa kuitekeleza.

chanzo:bbc.
Comments