SMZ yatakiwa kuviangalia viwanda vilivyokufa.

wawakilishiSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetakiwa kuliangalia tatizo la kufa kwa viwanda ambavyo vinawanyima fursa za maendeleo wananchi hususa vijana wanaokabiliwa na tatizo la ajira kwa muda mrefu.
Akiuliza swali katika kikao cha baraza la Wawakilishi huko Chukwani Nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar kuhusu kufufuliwa kwa kiwanda cha Mafuta kilichopo Buyu ,
Mwakilishi wa jimbo la Chukwani Mwanasha Khamis Juma amesema pindipo kiwanda hicho kitafufuliwa kitaweza kuwasaidia wananchi waliokizunguka kiwanda hicho.
Aidha amesema mbali na kufa kwa kiwanda hicho vipo viwanda mbali mbali vilivyokufa hapa Zanzibar lakini vimechelewa kufanyiwa matengenezo ya haraka na kupelekea wananchi kuchelewa kupata maendeleo katika shehia zao.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Nchi Ofisi ya ya Raisi Issa Haji Gavu amesema  kufa kwa kiwanda hicho kinatokana na Mradi uliokua unasismamia kiwanda hicho kushindwa kuendelea na shuguli walizozikusudia kwa kushindwa kukamilisha taratibu za uwekezaji.
Hata hivyo amesema serikali itaendelea kujikita katika kuweka utaratibu maalumu wa kusajihisha wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta ya viwanda Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia wananchi juu ya matatizo yanayowakili pamoja na wananchi kuweza kunufaika na rasilimali zilizopo.
chanzo:Zanzibar24.

Comments