SMZ: Taasisi binafsi na wazazi wanajukumu la kuwalinda watoto yatima.

wawakilishiSerikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesema taasisi binafsi na Wazazi wanajukumu kubwa la kuwasaidia watoto yatima waliopo katika jamii ili kupunguza uwepo wa watoto ombaomba wanaojiingiza katika vitendo hatarishi.
Akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Chonga Shaibu Saidi Ali ,katika kikao cha Baraza la wawakilishi huko chukwani Nnje kidogo ya Mji wa zanzibar kuhusu kudhurura kwa watoto yatima katika mitaa, Naibu wa Waziri wa Uwezeshaji ,Wazee ,Vijana, Wanawake na watoto
Shadya Muhammed Suleiman amesema kwa sasa kuna ongezeko kubwa la watoto yatima linalotokana na ongezeko la watu pamoja na vifo vya wazazi wao.
Aidha amesema mbali na watoto hao lakini pia kuna wimbi kubwa la watoto wanaokosa maandalizi mazuri kwa wazazi wao na kupelekea watoto hao kujiingiza katika ajira hatari pamoja na kushiriki katika vitendo vibaya ikiwemo uvutaji wa dawa za kulevya na uporaji wa mali za wananchi katika jamii.
Ametowa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kujenga uhusiano mzuri kwa watoto wao ili kuwaepusha kushiriki katika makundi hatari hali inayosababisha kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji wa watoto pamoja na kukosa haki zao za msingi ikiwemo kupata elimu.
chanzo:Zanzibar24.

Comments