SMZ: Mwezi mtukufu wa Ramadhani uheshimiwe.

Serikali ya Mapinduzi zanzibar  imesema itachukua hatua za kisheria katika kuhakikisha,heshima na hadhi ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani inalindwa ili kuitekeleza vyema ibada ya funga.

Akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Paje Jaku Hashim Ayoub Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Maalimu amesema miongoni mwa hatua zilizopangwa kuchukuliwa na serikali ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi maeneo mbalimbali pamoja na miskitini ya Ijumaa juu ya umuhimu wa kuupa heshima mwezi huo.

Hata hivyo Maalimu ametoa wito kwa wananchi  kujiepusha na matendo yote yatakayopelekea kuuvunjia heshima ya mwezi  wa ramadhani kama vile kula ovyo hadharani,kuvuta sigara,kutovaa vivazi vya heshma pamoja na kutoa maneno ya kumkashifu mwezi mungu.
Sambamba na hayo pia akizungumzia suala la utalii  amesema serikali itajenga mazingira bora kwa wageni kutoka nje ya nchi watakaokuja kutembea zanzibar  ili nawao wasije kuungia katika mambo yatakayopelekea kuukashimu mwezi huo licha ya kuwa wanafanya utalii.
chanzo:Zanzibar24

Comments