Serikali imetenga Sh30 bilioni (30) katika mwaka wa fedha 2017/2018 ili kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi wa Kipunguni wanaopisha upanuzi wa uwanja wa ndege.
Hayo yamesemwa leo (Jumanne) bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea , Bonnah Kaluwa.
“Ni kweli Serikali ilifanya uthamini wa mali za wananchi ili kupisha upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam mwishoni wa miaka ya 90 ambapo maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya upanuzi huo ni Kipawa,Kigilagila na Kipunguni”, amesema.
Ngonyani amesema kuwa kutokana na gharama za fidia na uhaba wa fedha Serikali imekuwa ikilipa fidia kwa wakazi hao kwa awamu.
chanzo:Mwananchi.
Comments