Serikali ya Zanzibar kuendeleza azma ya kujenga nyumba za ghorofa za makazi.

baraza-la-wawakilishiWizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji imesema itaendeleza azma yake ya kujenga Nyumba za ghorofa katika kisiwa cha Zanzibar ili kupunguza tatizo la uhaba wa ardhi unao wanyima fursa wananchi kuendeleza shughuli zao za kijamii ikiwemo kilimo.

Akijibu swali katika kikao cha Baraza la wawakilishi huko Chukwani nje kidogo ya Mjini wa Zanzibar Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mohammed Ahmada amesema serikali inaelewa tatizo la uhaba wa ardhi na kuanzisha sheria ya mwaka 2014 ya kuanzisha shirika la nyumba Zanzibar ili liweze kusimamia ujenzi wa Nyumba za Ghorofa.


Amesema katika kubana matumizi holela ya Ardhi hivi sasa Shirika la Nyumba linaendelea na mpango wake wa utekelezaji wa Ujenzi wa Nyumba za ghorofa kwa ajili ya kutowa huduma bora kwa wananchi.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi wameelezea wasiwasi wao juu ya kuwepo kwa matumizi holela ya ardhi ambapo wananchi wamekuwa wakijenga nyumba za kuishi bila kufuata sheria na kupelekea kupungua kwa ardhi katika kuendeleza matumizi mengine ya maendeleo.

chanzo: Zanzibar24.

Comments