
Saa chache baada ya Rais John Magufuli kumtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ajitafakari ikibidi ajiuzulu, tayari Rais ametengua uteuzi wake.
Mapema leo, Jumatano Rais Magufuli alimtaka Profesa Muhongo ajitathmini kuhusu nafasi yake ya uwaziri baada ya kupokea ripoti ya mchanga wa madini Ikulu.
Hata hivyo, kabla ya Profesa Muhongo kutoa kauli yoyote Rais ametengua uteuzi wake kuanzia leo.
Nafasi ya Profesa Muhongo itajazwa baadae.
chanzo:mwananchi.
Comments