
Mwenyekiti wa Kijiji cha Matwiga, Nehemia Muga amethibitisha kutokea
kwa kifo cha mtoto huyo huku walimu wa shule hiyo wakitoroka muda mfupi
baada ya tukio hilo kutokea.
Kwa upande wa wanafunzi waliokuwepo shuleni hapo walisema kuwa
“Mwalimu akaanza kuita mwanafunzi mmoja mmoja fulani aje hapa, unaulizwa
kama huna kosa unaenda kwahiyo hao wawili akawachukua mmoja alikuwa
anaomba msamaha akamkatalia akawachukua wanafunzi wawili akasema
mpelekeni huko baada ya kuwapeleka kwenye chumba hicho akawafungia na
kufuli.”
Matukio mbalimbali ya unyanyasaji wa wanafunzi Mkoani humo yamekuwa
yakiendelea baada ya wiki kadhaa kupita mwanafunzi wa Mbeya day
kuadhibiwa na walimu kwa kupigwa fimbo mfululizo.
chanzo: zanzibar24.
Comments