Mambo mawili wasio kubalina nayo ACT katika orodha ya watumishi wa serikali wenye vyeti vya kughushi.

actMwishoni mwa wiki, Rais John Magufuli alipokea orodha ya watumishi wa serikali 9,932 kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, ambao wamejipatia ajira kwa vyeti vya kughushi.

Orodha ambayo ilikua na wafanyakazi wengi kutoka katika hlmashauri na wachache kutoka katika taasisi nyegine za serikali na mashirika ya umma.

Chama cha ACT wazalendo kinonesha kuunga mkono kwa uamuzi wa serikali kuwachukulia hatua watumishi wote wa umma waliobainika kutumia vyeti feki ikiwemo kuwafukuza kazi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.


Katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu, inabainisha kuwa bila shaka hatua hiyo itapanda mbegu ya uwajibikaji, kuchochea uadilifu na kuhakikisha uweledi kwenye utumishi wa umma.

“Mbali na kupongeza, yapo masuala kadhaa yaliyoibuka kwenye uhakiki huo ambayo tunadhani hayakwenda sawasawa na hivyo basi sisi kwa nafasi yetu tunao wajibu wa kuyakemea ili kuufanya mchakato huu uende kwa haki,” alieleza Shaibu.

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu, inabainisha kuwa bila shaka hatua hiyo itapanda mbegu ya uwajibikaji, kuchochea uadilifu na kuhakikisha uweledi kwenye utumishi wa umma.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni kitendo cha Rais John Magufuli kuwasamehe wale watakaojiondosha kazini wenyewe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale watakaoendelea kubaki kwenye nafasi zao jambo ambalo ni kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi.

Alisema kisheria Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu anayetuhumiwa kufanya kosa la jinai iwapo mtu huyo hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuhukumiwa. “Madaraka pekee aliyonayo Rais ni kutoa Msamaha kwa wafungwa wanaotumikia kifungo kama alivyofanya hivi karibuni kwenye Sherehe za Muungano,” alisema.

Aidha, alitaja jambo jingine ambalo chama hicho hakikuridhika nalo kuwa ni madai ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, kuwa mchakato wa uhakiki wa vyeti haujawagusa wanasiasa na wateule wa rais kwa sababu cheti si sifa ya kupatikana kwao.

“Ikumbukwe kuwa msingi wa utaratibu huu ni kuhakikisha kuwa taifa linabaki na watumishi wenye sifa. Waziri Kairuki anasema kuwa sifa pekee ya Kikatiba ya Viongozi wa kisiasa ni kuwa wajue kusoma na kuandika.

Waziri hakutaka kujiuliza iwapo viongozi wa kisiasa watathibitika kughushi vyeti ambalo ni kosa la jinai haitawaondolea sifa yao ya uongozi? alihoji. 

Alimshauri waziri huyo mwenye dhamana ya utawala bora kuona kuwa uhakiki wa vyeti kwa viongozi wa kisiasa na wateule wa rais kama vile mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ni muhimu kwa kuwa unakwenda sambamba na viapo na matakwa ya kimaadili.
Chanzo: HabariLeo na zanzibar24.

Comments