Makamba kubisha hodi kwa Profesa Muhongo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba amesema atamuandikia barua Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ili apate wataalamu wa miamba  kwa ajili ya kutafiti  miamba iliyoachia katika milima ya Lushoto.

Akizungumza baada ya kukagua barabara ya Soni –Mombo, Makamba amesema hatari  iliyopo ni kuporomoka kwa udogo  kutoka kwenye milima, kuachia kwa miamba na kuporomoka kwa mawe makubwa jambo ambalo  miaka ya nyuma halikuwepo.

Waziri huyo amesema  ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea amekusudia kuomba wataalamu kutoka kitengo cha Jiolojia kilichopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini  ili waende kukagua na kutoa  ushauri juu ya kuachia kwa miamba hiyo.
Makamba amesema kuwa kudondoka kwa mawe makubwa kutoka katika milima hiyo kulianza mwaka juzi  wakati wa msimu wa mvua.
chanzo:Mwananchi.

Comments