Huku akiwakazia macho maofisa ardhi wa jiji, Lukuvi alihoji sababu za idara hiyo kuwabana wananchi wa kawaida na kuwafumbia macho viongozi wa Serikali na kisiasa wanaodaiwa kodi na ushuru wa ardhi.
Akizungumza kwa simu kuhusu deni hilo Mansoor alisema suala la ulipaji wa kodi ya eneo hilo liko mahakamani tangu mwaka jana ingawa upande wa pili ambao ni halmashauri haujitokezi kwenda kusikiliza.
Alisema eneo hilo limezungukwa na mlima uliojaa mawe makubwa na kwamba ni ekari tano pekee ambazo anatakiwa kuzilipia kodi.
“Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikifuatilia halmashauri ya jiji ili kubadilishiwa hati kwa kuwa eneo linalofaa kuendelezwa ni ekari tano pekee, zilizobaki ni milima ambayo haipaswi kuiendeleza isipokuwa kuchimba mawe kwa ajili ya ujenzi au kuponda kokoto,” alisema Mansoor.
chanzo:Mwananchi.
Comments