Kiongozi huyo ni Ismail Haniyeh ambaye hadi hivi karibuni alikuwa ndio kiongozi wa kundi hilo katika ukanda wa Gaza.
Akijulikana
kama kiongozi anayetumia akili nyingi wakati wa kutatua maswala,
anachukua mahala pake Khaled Meshaal ambaye ameliongoza kundi hilo akiwa
ughaibuni kwa miongo miwili.
Uchaguzi wa kiongozi mpya ulifanyika
kupitia njia ya Video Link kati ya wajumbe waliopo katika ukanda wa
Gaza na wale waliopo nchini Qatar ambako Meshaal ana makao yake.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa bwana Meshaal anaachia ngazi wakati ambapo Hamas limeanza kulegeza msimamo wa kisiasa.
Kwa mara ya kwanza wiki iliopita katika sera mpya kundi hilo liliwachilia wito wake wa kuiharibu Israel.
Hamas
bado lina wapiganaji wake katika eneo la Gaza na bado linaaminika kuwa
kundi la kigaidi na Israel Marekani na mataifa ya bara Ulaya.
chanzo:Bbc.
Comments