
Akizungumza
na mwandishi wetu kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba Ali Haji
amewataja wanaotuhumiwa na tukio hilo kuwa ni Riziki Juma Makame, Khamis
Hamad Ali na Chumu Matari.
Kamanda Haji amesema tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku wa kuamkia siku ya ijumaa katika msitu wa mjini Wingwi.
Ameeleza
kwamba jeshi la polisi lilipata taarifa hizo kutoka kwa raia wema na
ndipo walipochukua hatua za kijeshi nakufanikiwa kuwatia mikononi
watuhumiwa hao.
“Tunaendelea kuwahoji watuhumiwa, ambao ni baba wa mtoto, mama pamoja na bibi wa mtoto”amesema kamanda Haji
Licha
ya watuhumiwa wakike kushindwa kuzungumzia tukio hilo lakini baba
anayetuhumiwa kuhusika amekiri na kusema kuwa yeye ametumwa na mama mkwe
wake amtupe mtoto huyo na sio kuuliwa.
Akizidi
kuelezea mkasa huo amesema kua yeye hakusika na kitendo cha kuuwa na
kwasababu hakushirikishwa hata kidogo katika mpango huo na kwamba
angeshirikishwa asingekubali kufanya hivyo.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya micheweni Abedi Juma Ali ameelezea
kusikitishwa na tukio hilo na kuviomba vyombo vya sheria kuchukua hatua
kali kwa watakao bainika kuhusika na tukio hilo.
Amesema
serikali ya wilaya pamoja na vyombo vyake vya ulinzi vitaendelea
kushirikiana na wananchi katika kusimamia haki za watoto ili zisikiukwe .
Naye
afisa ustawi wa jamiii wilaya hiyo Hamadi Othmani amesema pamoja na
elimu inayotolewa na ofisi yake lakini bado baadhi ya wananchi
wanaipokea kwa mtizamo tofauti.
Hili
ni tukio la kwanza kutokea katika wilaya ya micheweni ya mtoto
kuzawaliwa na kuuliwa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na kisha
kutupwa msituni.
chanzo: zanzibar24.
Comments