Famili za ndugu walio potea baharini msuka Pemba wafariji.

Wavuvi wanne wahofiwa kufa katika bahari ya Msuka PembaWAFANYAKAZI wa Idara ya maendeleo ya Uvuvi Kisiwani Pemba, wamewafariji ndugu na jamaa wa familia waliopotelewa na ndugu zao huko baharini kutokana na shughuli za uvuvi.

Wavuvi hao wakaazi wa Msuka, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa kaskazini, walikwenda baharini siku ya Jumaapili ya tarehe 21 hadi leo bado hawajaonekana.

Wavuvi wenyewe ni Khamis hamad Sharif (40), Mbarouk Said Juma (58), Hamad Abdalla Salim (28), na Ali Abdalla Khamis (52).


Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, ndugu wa karibu wa familia wamesema kuwa, jitihada za makusudi zimekuwa zikifanywa kwa karibu kwa ushirikiano na viongozi mbali mbali wa Serikali na Wanajamii kwa kutumia usafiri wa baharini kuwatafuta ndugu zao bila ya mafanikio yoyote hadi sasa.


Mmoja kati ya Maofisa wa Uvuvi waliofika kijijini hapo Nd.Hidaya Khamis Hamad, amewataka wanafamilia hao kwa nyakati tofauti kuwa wastahamilivu katika kipindi hichi  na kuendelea na jitihada za kuwatafuta huku Idara ya Uvuvi nayo ikiwa pamoja nao kwa karibu kwa hali yoyote itakayotokea.

Comments